IQNA

Turathi za Kiislamu

Nakala za kale za Qur’ani zinazoonyeshwa kwenye Jumba la  Makumbusho la Kazan

22:03 - May 26, 2024
Habari ID: 3478887
IQNA - Msururu wa nakala za kale za Qur’ani Tukufu na athari za Kiislamu zimeonyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Kazan katika mji mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan ya Shirikisho la Russia.

Zinajumuisha nakala kadhaa za Misahafu ya Kale, kulingana na tovuti ya Al-Masry Al-Yawm.

Mojawapo ni nakala adimu ambayo ni ndogo kiasi kwamba mtu anahitaji miwani maalumu ili asome aya hizo.

Jumba la makumbusho pia lina athari za kihistoria za tangu  enzi ya Watsar nchini Russia na  Vita vya Kwanza vya Dunia.

Ni moja wapo ya vituo vikubwa zaidi vya kitamaduni na kihistoria katika mkoa wa Volga katika wilaya ya zamani ya Kazan.

Mji mkuu wa Tatarstan ni kituo kikuu cha Waislamu nchini Russia na ni moja ya miji ya kwanza katika ulimwengu wa Kiislamu ambapo nakala za Qur’ani zilichapishwa.

Mus’haf Kazan ni miongoni mwa nakala kongwe zaidi zilizochapishwa za Qur’ani Tukufu katika Uislamu. Ilichapishwa na lithography mnamo 1803 katika saizi mbili.

Ni nakala chache tu za Mus’haf wa kale ambazo zimesalia, moja ambayo imehifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Kazan.

3488499

Kishikizo: russia na uislamu
captcha